Mwenye Wivu Hashindi

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Hapa duniani kuna watu ambao shughuli zao kubwa ni kukatisha tamaa wenzao katika mambo mbali mbali wayafanyayo. Hiyo inatokana na roho ya wivu waliyonayo. Watu wa aina hii huwa hawawezi kumsifia mtu hata kama amefanya jambo zuri. Watu hawa huwa wako tayari kukukatisha tamaa ili ionekane ulichokifanya hakina maana yoyote ile.
Usemi huu unatufundisha kuwa na usiri wa mambo tuyafanyayo. Siyo vizuri kutangaza kwa kila mtu kile ufanyacho. Hii ni kwa sababu mtu mwenye wivu huwa hapendi maendeleo ya mtu mwingine. Mara nyingi, mtu mwenye wivu, hupenda kulifanya jambo lile lile ambalo amekukatisha nalo tamaa wewe. Lakini kwa vile halikuwa wazo lake, atashindwa kulifanikisha.
Ukweli ni kwamba mtu hawezi kuendeleza ama kufanya jambo ambalo limetokana na wazo la mtu mwingine kwa sababu halikutoka kichwani kwako. Ataweza kuiga lakini mwisho wa siku, atashindwa. Hatimaye ataishia kuliacha, na nyote mkakosa.
Mtu mwenye wivu ni wa ajabu sana, kwani mnapokosa wote hiyo ndiyo inakuwa furaha yake kubwa. Tunaaswa kuwa waangalifu na watu wa namna hii, watatupoteza. Tuache kutangaza kwa watu kila tufanyacho, kwani hatuwajui undani wao. Tungojee tukifanyacho kikamilike kwanza ili kukwepa kukatishwa tamaa tukiwa katika na hata mwanzo wa safari. Yatupasa tuzingatie ushauri huu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection