Kulia Kupokezana

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Wako watu wenye tabia mbaya za kuchekelea au kufurahia wenzao wanapopata matatizo au changamoto katika maisha yao. Watu hawa hujisahau na hukosa ufahamu kwamba, hapa duniani, matatizo huwa ni ya mzunguko. Hii ina maana kuwa leo yakiwa kwa mwenzio kesho yatakuwa kwako, na kesho kutwa kwa mwingine. Maisha ndivyo yalivyo, tusijisahau.
Mfano hai ni kifo. Kifo hakizuiliki kutokea, iwe kwako au kwa mwingine. Kama kutokea kitatokea tu, kwani sisi hatupangi kupata misiba, bali unajikuta imetokea tu.
Kwa hiyo kama utakuwa unafurahia matatizo ya wenzio, na pia unakuwa huna ushirikiano wa karibu nao, nawe ukae ukijua kwamba zamu yako ya kufika itakapofika, utajikuta uko peke yako. Utakosa mtu wa kukufariji. Kwa hakika unaweza hata ukachanganyikiwa kwani wakati huo ndio unahitaji kuwa na watu karibu yako, watu ambao watakukumbatia na kukufanya upunguze mzigo mzito ilipofika moyoni mwako.
Hivyo basi, tunaaswa tuwe na tabia ya kushiriki katika shida au furaha za wenzetu katika jamii inayotuzunguka ili nasi tutakapopata shida au furaha tuweze kuwa na watu ambao watakuwa tayari kuwa nasi wakati wote wa raha ama shida zetu.
Sisi binadamu, tunaishi kwa kutegemeana. Hakuna binadamu hata mmoja aliyekamilika. Msemo wa ‘Umoja ni Nguvu, Utengano ni Udhaifu,’ unasisitiza zaidi nadharia hii. Ushirikiano unapunguza mambo mengi yanayotusibu sisi binadamu. Kuna watu husema, asiyependa ushirikiano, ni mchawi. Je ni kweli usemi huo? Tafakari.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection