Kama Hukushiba Kwenye Tonge, Kwenye Kulamba Utajisumbua Tu

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Mbiu ya maisha huanzia mapema. Kama mwanzo wa safari yako haukuwa mzuri, unaweza ukafika uendako kwa matatizo au kwa shida sana.
Mafanikio yana mahali pa kuanzia. Jitahidi mwanzo wako uwe mzuri kwa vile huko uendako hukujui. Kunaweza kukawa ni kugumu na hasa pale unapokosa kuwa makini. Mwanzo wako ukiwa mzuri na huko uendako kunaweza kukawa kwepesi, lakni hiyo inategemea pia.
Ndio maana ya usemi huu, ugumu uko mwanzo lakini mwisho kunaweza kukawa sawa na mteremko yaani mambo yako yakakuwia mepesi.
Pale maisha yanapokuwa mazuri na mepesi unaweza ukasahau kule ulikotoka. Matatizo yote uliyopitia, yatasahaulika.
Sana sana, utajikuta unawatia moyo watu kwa kuwasimulia mambo yako ya kule ulikotokea. Maisha ndivyo yalivyo. Kila mtu ana mapito yake hapa duniani. Yatupasa tuwe tayari kuwamegea wenzetu mapito yetu hususani yaliyotufikisha kwenye mafanikio ili yawe mafunzo kwao pia.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection