Bandu Bandu Humaliza Gogo

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Maisha ni safari ndefu sana ambayo imejaa mapito mengi mazuri na mabaya. Unaweza ukapitia eneo ambalo ni la kukukatisha tamaa hata ukakosa jawabu.
Unaweza ukaanzisha biashara kwenye eneo fulani ukiwa peke yako lakini baada ya muda mfupi watu wengi watakuja na kuanza biashara kama ile ya kwako. Hali hiyo inaweza ikakushitua unapoona kuwa wao wanauza zaidi yako. Katika hali hiyo lazima utakata tamaa na kusononeka.
Yakupasa usiangalie hayo, kidogo unachopata ridhika nacho, maadam ndicho kilichopangwa na Muumba wako. Endelea tu, utafika mahali, utakuwa sawa. Kidogo kidogo nndio mwendo. Kumbuka kuwa hakuna jambo linaloanzia juu bali kila ulifanyalo linaanzia chini kwenda juu.
Usemi huu unafundisha umuhimu wa kujiwekea kidogo kidogo kama akiba kwa matumizi ya baadae. Sawasawa na usemi huu, ni ule usemao haba na haba hujaza kibaba. Hata hawa matajiri wakubwa walianza chini na hatimaye wakafanikiwa kufikia walipo sasa hivi.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection