Zuia Mawazo Hasi.

Simulizi
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Upo ule wakati kwenye maisha yako unaona kama umefika mwisho kabisa.
Yaani, kila ukijiangalia unaona kabisa hauna nguvu tena za kuendelea mbele.
Ni wakati ambao, hata wale ambao uliwahesabu kuwa ni watu wako wa karibu sana huwaoni tena.
Ni wakati wa maumivu na ukiwa mtupu.
Ni wakati ambao, unaona kabisa ndoto zote ulizokuwa nazo ni kama zimefikia mwisho. Wakati mwingine, unajikuta unatoa machozi tu ukiwa peke yako.
Ni rahisi sana kuanza kujiuliza nimekosea wapi na kuanza kujilaumu kwa yaliyopita.
Namna nzuri ya kukabiliana na wakati huu ni kuzuia mawazo hasi. Badala yake ni kujenga imani ya kuwa hili nalo litapita, nitavuka salama. Kumbuka, kila jaribu lina mlango wa kutokea. Kamwe hutakiwi kukata tamaa.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection