Jitie Moyo Kila Wakati!

Simulizi
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Haijalishi unapitia changamoto gani kwenye maisha yako, jitahidi kupata muda wa kujipa moyo. Kama ni chakula kula vizuri mlo kamili ili usiidhuru afya yako halafu ukasababisha magonjwa sugu.
Pia pata muda wa kujijali yaani jipendezeshe kuoga na upake mafuta yako ung'are na uvae vizuri.
Sio vizuri unapopita kwenye changamoto basi kila mtu ajue kuwa unapitia pagumu kwa mwonekano wako wa nje. Usikae muda wote unawaza changamoto zako, usijifungie na kuanza kulia muda wote, usijifungie na kusikiliza nyimbo za huzuni, bali sikiliza na kuziimba nyimbo zinazoonesha ukuu wa Mungu ili zikuongezee matumaini.
Epuka kusimulia matatizo yako kwa kila mtu. Shirikisha mtu mmoja unayemuamini na sio watu wako wote kila anayekupigia simu unaeleza shida zako.
Kumbuka hakuna lidumulo hata kama changamoto ni kubwa na ngumu kiasi gani, uwe na uhakika itafika mwisho. Jipe muda. Wahenga walinena, hata kama usiku ni mrefu sana lazima kutapambazuka tu, hata iweje.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection