Usifanye Maamuzi Kwa Ajili Ya Leo Tu, Angalia Na Kesho Yako.

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Usibamize mlango wakati wa kuondoka. Ukifunguliwa na mtu /watu mlango uliouhitaji siku ukitaka kuondoka usiubamize huo mlango kwa nguvu , huenda kesho ukahitaji kuutumia tena wakati wa kuingia.

Kwenye maisha kuna wakati watu huwa wanatufungulia milango na milango hiyo huwa ni ya kutufaa sana wakati tunapoingia, lakini mara nyingi tukishaingia ndani kupitia mlango ambao watu kwa upendo na mapenzi mema walitufungulia, baadaye tukishapata mlango ulio bora zaidi au tukishapata kile tulichokuwa tunakitaka ndani, huondoka kwenye ule mlango wa zamani kwa kuubamiza sana na kwa namna isiyo nzuri.

Jambo la kujifunza hapa ni kwamba, umuhimu wa mtu kwenye maisha huwa hauishi ila tu kwa muda fulani fulani huenda majira yakaisha. Hivyo kama mtu hakukufaa masika haimanishi wakati wa kiangazi hatakufaa.
Wakati unamwendea yule unayeona kuwa atakufaa kwa masika yule mwingine achana naye kwa amani, jitahidi sana kutengeneza amani na mtu iwapo kuna mazingira yatawalizimu kuachana kwa muda.
Lakini niamini huyo ambaye alikufaa juzi, leo asipokufaa haimanishi kuwa hatakufaa milele, ni kwa majira tu, hivyo kama imekubidi kuondoka kwake na kutengana naye basi tumia hekima kubwa sana wakati wa kutengana. Usimjeruhi moyo wake katika viwango ambavyo kesho ukimuhitaji hatakuwa tayari kukusaidia tena.
Usiubamize mlango, huenda kesho ukahitaji kutumia tena mlango huo kuingia.


The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Jitie Moyo Kila Wakati!

Next
Next

Elewa Kusudi La Kuwepo Kwako!