Elewa Kusudi La Kuwepo Kwako!

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Uwepo wa kila mtu unakuwepo tokea mtu akiwa tumboni mwa mama yake. Hivyo ulivyo sasa ni kusudi ambalo ulizaliwa nalo. Kutokana na hali hiyo unatakiwa kujua kusudi lako ili uweze kupanga namna ya kupata mafanikio.

Kusudi ni mwongozo au dira ya maisha ya mwanadamu. Dira inamsaidia mtu kupanga mikakati yake. Fahamu kuwa chochote unachokifanya kiko ndani ya kusudi ulilonalo. Ukifanya jambo ambalo halipo kwenye kusudi lako mara nyingi huwa halifanikiwi

Ukilijua kusudi lako utajua thamani ya maisha yako. Kusudi linakuongoza kwenye mafanikio na ndoto zako. Yakupasa uishi kulingana na kusudi lako. Hapo itabidi utambue kusudi lako la kuwepo hapa duniani.

Mara nyingi kwenye kusudi lako kunainuka vita ili kukutoa na kukukatisha tamaa. Unapoona vita vinainuka kwenye jambo lako au nafasi yako basi elewa hilo ndilo kusudi lako na kwamba wanataka kukutoa kwenye mafanikio yako. Usikate tamaa pambana ili ushinde..
Kumbuka, majaribu ni mtaji wa mafanikio ya mwanadamu yeyote.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Usifanye Maamuzi Kwa Ajili Ya Leo Tu, Angalia Na Kesho Yako.

Next
Next

Kaa Mbali Na Wenye Fikra Hasi, Kwao Hakuna Jema!