Kaa Mbali Na Wenye Fikra Hasi, Kwao Hakuna Jema!

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Watu wenye fikra hasi ni wale wanaopenda kukatisha tamaa wenzao kwa kila wanalolitenda. Wao kazi yao ni kukandamiza tu wenzao na pia ni kujaribu kwa kila hali kufuta maono ama ndoto za wenzao.
Katika hali hiyo usiposimama imara, wao watatumia misimamo yao ili kukutoa kwenye reli na kwenye malengo yako. Sana sana wanaweza wakakuambia, “ mbona mimi nilifanya hivyo na sikufanikiwa, sasa wewe unafikiri utaweza”? Kumbe lile jambo yeye wala hajawahi kulifanya wala hata kulijaribu. Amelijua pale wewe ulipolifanya na kushangaa kuona umefanikiwa. Hapo ndipo inathibitisha dhahiri roho mbaya na wivu wa watu dhidi ya mafanikio yako.
Maandiko matakatifu yamesema, “furahia mwenzio anapopata, nawe subiri siku yako”. Muumba wetu amuwekea kila mtu na siku yake. Kama ambavyo hatujui siku wala saa ya kuondoka hapa duniani, ndivyo ilivyo kwenye mafanikio yetu. Nyakati na majira yakifika, hakuna mtu anaweza kuzuia.
Usemi huu unatufundisha kuchagua marafiki wema ambao hawawezi kutuangusha ama kutuyumbisha na kututoa kwenye reli. Binadamu wengine si wema kabisa. Wachunguze sana na hasa maneno yatokayo midomoni mwao. Unaweza ukawajua tu wabaya wako.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection