Huwezi Kupata Kivuli Kwenye Mti Uliopinda!

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mti ni nishati ambayo ina matumizi mengi sana. Kwenye mti tunapata matunda, tunapata mbao, kuni na hata dawa. Wengine hupanda miti kwa ajili ya kivuli, hususan kwenye maeneo ya kuzunguka makazi yao.

Hapa tunazungumzia mti na kivuli kama ushauri katika maisha kwenye jamii zetu. Unapotaka kupata ushauri lazima uangalie ni nani ambaye anaweza kukushauri katika hilo jambo ambalo linakusumbua. Vile vile unatakiwa uangalie hata umri wa mtu unaemuendea kwa kupata ushauri.

Tahadhari hii inatolewa kwa sababu wapo watu ambao ukiwapelekea shida yako anaweza akakuzidishia tatizo badala ya kulipunguza. Hiyo ndio maana ya usemi huu wa mti uliopinda ambao hautoi kivuli kizuri.

Kuna watu ambao wana hekima ya kuweza kushauri. Hao ndio tunawaita mti ulionyooka wenye kivuli kizuri. TEWWY imechukua akina mama watu wazima ili waisaidie jamiii, hususan vijana ili kutatua matatizo yao ya kimaisha. Sababu ya kuwachukua akina mama hawa ni kutokana na ukweli kuwa wamepitia kwenye mambo mengi ya maisha na hivyo hakuna jambo gumu kwao la kushindwa kulitolea ushauri .

Kwa hiyo tunawasihi vijana na jamii mzima kwa ujumla, kuwa makini katika kutafuta ushauri maana wengine wanaweza kuwa ni miti iliyopinda.

Usemi huu unawahusu vijana pamoja na wote wenye shida ya kupata ushauri. Inawapasa muangalie ni nani wa kumpa shida zenu kwa ajili ya kupata ushauri ili msije kudhalilika.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Kaa Mbali Na Wenye Fikra Hasi, Kwao Hakuna Jema!

Next
Next

Usitengeneze Kundi La Kumchukia Mtu Kwa Chuki Zako Binafsi!