Usitengeneze Kundi La Kumchukia Mtu Kwa Chuki Zako Binafsi!

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Ulimwengu huu umejaa shida na vurugu tele kila uchwao. Karibia kila siku tunakutana na mambo mengi mazuri na mabaya pia. Mambo yaliyo
mabaya hutokana na mahusiano katika jamii nyingi. Migongano ya mtu na mtu au kikundi na kikundi, ni mambo ya kawaida katika maisha tunayoyapitia.

Kuna tabia iliyojengeka kwenye jamii zetu ya mtu kumchukia mwingine kwa jambo dogo tu ambalo lingeweza kuongeleka. Katika hali hiyo watu wamejenga tabia ya kulishawishi kundi moja ili na wao wamchukie yule wasiyempenda. Kwa tabia hii, utakuta wengi
wanaingia kwenye ugomvi usiowahusu.

Kwa mfano, hivi karibuni wengi wetu tuliingia kuisema serikali kuhusu uwekezaji kwenye bandari. Bila hata ya kuelewa nini kinachoendelea tulijikuta tunaingia kwenye kulaumu jambo ambalo hatulielewi vizuri. Hiyo ilitokana na kundi fulani kutuaminisha yale wayasemayo na hivyo wao kujiona kuwa wanaelewa zaidi kuhusu suala hilo.

Wengi wetu tulikuwa hatujui tunachokipinga ila tu, kwa sababu walituaminisha hivyo Pamoja na kuwa tulisema sana lakini hakuna kilichobadilishwa. Wengi tulibaki na maumivu yetu na kuwa na maswali mengi yasiyo na majibu.

Kutokana na hayo, tunafundishwa umuhimu wa kuwa makini kwenye mambo
yanayozungumzwa na yasiyo tuhusu.
Sambamba na hilo, hatutakiwi kuingilia ugomvi uliopo baina ya wana ndugu. Daima kumbuka kuwa siku wakija kupatana, hawatakushirikisha.
Utaishia kupata aibu na kujilaumu. Zaidi ya yote, wewe ndio utaonekana kuwa ni
mchonganishi. Yatupasa tuepukane na mambo yasiyotuhusu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Huwezi Kupata Kivuli Kwenye Mti Uliopinda!

Next
Next

Mtenda Wema Ana Malipo!