Mtenda Wema Ana Malipo!

Simulizi
Wema ni tendo la kumkirimu mtu au kumsaidia pindi anapopatwa na matatizo. Msaada huo unaweza kuwa wa kuombwa ama wa hiati, pale roho yako inapoamua kumsaidia mhitaji.
Inawezekana mtu kaguswa na hali aliyoiona na akalazimika kusaidia ili aondokane na changamoto aliyokuwa nayo. Lakini inafika wakati msaada huo unakuja kuwa wa kumdhalilisha mtu maana kila wakati mtoaji anauongelea. Yaani inakuwa kama vile masimango. Tabia hiyo siyo nzuri kabisa.
Tunafundishwa kuwa, daima unapotenda wema usingojee shukurani bali wewe usubirie malipo yako maana kila mtenda wema ana malipo yake. Tatizo letu kubwa huwa ni kutegemea yule uliyemsaidia, naye akusaidie. Kamwe huo sio mpango sahihi. Tenda wema uende zako nawe utakuja kutendewa mema na mtu usiemtegemea. Hivyo ndivyo maisha yetu yanavyokwenda kwetu sisi wanadamu.
Hatutakiwi kuwa watu wa kujitangaza kuhusu utoaji wetu. Riziki yako iko mbele yako, uwe na subira, malipo yako yahusuyo utoaji wako yako njiani.by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection