Usihukumu Kitabu Kwa Ganda La Juu.

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

Katika maisha yetu sisi binadamu tuna mambo ya kudharauliana sana. Hiyo inakuja kwa sababu ya kutokumuelewa mtu kwa undani wake. Inatokea pengine mtu kwa kukuangalia tu anakutafsiri kwa jinsi anavyokudhania yeye.
Tatizo kubwa ni kwamba mtu anashindwa kuelewa kitu kilichomo ndani yako, kitu ambacho yeye hana fununu nacho..

Kuna kusudi lililopo ndani ya mtu ambaye wewe unayemtafsiri huna, na pengine kamwe hutaweza kuwa nalo. Na kupitia hilo.kusudi alilonalo mwenzio linaweza kukusaidia hata wewe sikumoja. Hapo ndipo utasikia wakisema, ‘hivi ni yule yule au mwingine’.

Tunashauriwa kutomuangalia mtu kwa jinsi anavyoonekana. Huyo mtu anaweza kuwa na kitu au jambo la kuweza kukusaidia. Kila mtu inabidi aheshimiwe kwa vile alivyo. Hata mfagiaji naye inabidi aheshimiwe kwa sababu bila yeye mahali hapo mlipo pasingeweza kukalika bila yeye kutokana na uchafu utakaokuwepo. Kila mtu inabidi aheshimiwe, haijalishi anafanya kazi gani. Tutambue na kuheshimu mgawanyo wa majukumu ya kila mtu ili kukamilisha kilichopangwa kufanyika.

Usemi wa usihukumu kitabu kwa ganda la juu ni sahihi kabisa kutumika katika maisha yetu. Ukitaka kujua uzuri au ubaya wa kitu, inakupasa ufungue ndani ili uone kilichomo.

Kutokana na usemi huu tunajifunza kuacha kudharauliana kwa hali yoyote iwayo. Kila mtu ana muhimu kwako. Daima kumbuka kuwa heshima ni kitu cha bure, hakihitaji shule.

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Mtenda Wema Ana Malipo!

Next
Next

Uvivu Ni Adui Wa Mafanikio