Maji Hayasahau Ubaridi.

Simulizi
by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).
Kwa kawaida maji huchemshwa ili yawe ya moto. Lakini taratibu maji hayo hupoa na kurudi kwenye uhalisia wake. Vivyo hivyo, tabia ya mwanadamu huwa haiwezi kujificha kwa muda mrefu bila kurudi kwenye uhalisia wake.
Katika maisha ya sasa hivi ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu ya tabia ya kuigiza. Kijana wa kike anapokuwa kwenye mahusiano na kijana ambaye ana uwezo wa kimaisha, kabla ya kufunga ndoa ataigiza tabia ya upendo mpaka yule kijana atakiri kuwa amempata mwanamke sahihi wa kuishi naye milele. Atakuwa mkarimu kwa wazazi wa kijana. Na wazazi nao watasema huyu ni mwanamke wa kuoa.
Hali hii ya kuigiza itaenda hadi siku ya kufunga ndoa.
Sasa baada ya harusi anaingia ndani kwa mumewe halali.
Ataanza kuweka masharti kidogo kidogo. Utasikia akisema, fulani sipendi aje hapa kwa sababu ni mchawi. Hali kadhalika, na wazazi wako hawatakiwi kuja mjini kwani hakuna bajeti yao. Mara atakurupuka na kusema usiwatumie hela kila mwezi. Na ukituma, usitume
zaidi ya sh.10,000/= na hiyo iwe baada ya miezi mitatu.
Hatimaye anakurupuka kwa kusema anataka mfanyakazi wa kumsaidia kazi. Mwanaume anaweza akasema kipato chake hakitoshi kuweka mfanayakazi. Hali inazidi kuwa mbaya zaidi pale anapodai kukabidhiwa mshahara wa mumewe ili aweze kupanga matumizi ya nyumbani. Sababu ya kutaka mtumishi wa ndani inatokama na uvivu wake. Uvivu ndio tabia yake halisi. Mbaya zaidi huyu mwanamke ni mwongo, mchonganishi na mchoyo.
Hapo kijana anaanza kujilaumu na pale anapowajulisha nyumbani kwao nia yake ya kutaka kumuacha mwanamke huyu, wazazi wake wanakuwa hawamuelewi kabisa.
Kinachofuata yule kijana anatemgwa na familia na hata marafiki zake.
Katu hawaamini kama yule mwanamke aliyekuwa na adabu njema kabla ya kuolewa kuwa anaweza kufanya hivyo. Mwisho wa kijana huyu unaweza kuwa kutengana au kujiua.
Ushauri kwa vijana wote, wa kile na wa kiume ni kwamba kabla hamjaamua kuingia kwenye mahusiano, mjitahidi kupata historia za mtu huyo kutoka kwa ndugu na marafiki zake. Pia mpeleleze ukiwa mbali naye kwa takribani miezi 6 na huku ukimshirikisha Mungu. Kwa kufanya hivyo, utaweza kujua uhalisia wa tabia yake ya kweli na siyo ile ya kuiigiza.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection