Mafanikio Ni Mchakato!

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kwa kawaida binadamu huwezi kuhesabu mafanikio yako ukiwa umekaa au umebweteka tu. Kama ilivyo kawaida, siku huwa zinabadilika na kila siku ina mambo yake, na mafanikio vivyo hivyo. Lazima upitie mchakato ili uweze kufanikiwa. Endapo mchakato utaonyesha kukukwamishia mafanikio yako, basi elewa huo sio mchakato sahihi. Cha msingi, usikate tamaa endelea kuangalia mchakato mwingine. Unaweza hata kumshirikisha mtu ambaye unamuamini ambaye anaweza akakusaidia kwa mawazo au hata kwa mtaji.
Mchakato sio mteremko bali ni mlima mrefu ambao inabidi uupande ili uweze kufika kileleni kwa mafanikio. Wengi wetu huwa tuna tabia ya kukata tamaa tunapokutana na changamoto. Lakini hizo changamoto ni mtaji tu kwani hakuna jambo lisilokuwa na changamoto.
Kumbuka, changamoto ni mojawapo ya njia za kupita kuelekea mafanikio. Yatupasa tuwe makini kwa hilo, maisha ndivyo yalivyo.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection