Kipimo Chako Siku Zote Ni Ufanisi.

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Binadamu wote tumeumbwa tofauti katika nyanja nyingi. Wengi huwa wana ile hali ya kutaka kueleweka au kutambulika hata kama hawana jambo la maana walifanyalo. Kama ule usemi wa debe tupu haliachi kutika ndivyo ilivyo kwa wengi katika jamii zetu.
Wengi huwa wanapenda kuonyesha uwepo wao kwenye jamii husika. Hata katika sehemu ya kazi wapo watu ambao hupenda kujiweka mbele ili waonekane kwa viongozi. Watu kama hawa huwa wako tayari kusema mabaya ya wenzao na kuacha mazuri ambao wanafanya kwa lengo tu la kuwaharibia na kuwafanya wasionekane. Hata hivyo, ufanisi wa mtu ndicho kipimo pekee cha kumtambulisha kwa wakuu wake wa kazi. Watu wengi watakujua kutokana na ufanisi wako katika kutenda kazi zako ulizopewa kuzifanya. Zaidi ya yote, ni pamoja na utii utakaoonyesha kwa viongozi wako.
Mfano sisi wana tewwy tumekubaliana kutoa busara zetu na kiongozi wetu anatukumbusha mara kwa mara. Yatupasa tujitathimini na kujiuliza, je tunaenda kama vile tulivyokubaliana? Endapo hatufanyi vile tunavyopaswa, basi tujue kuwa tunamkosea kiongozi wetu na tunaweza tukasema tunakosa utii. Je kipimo chetu kitaleta ufanisi?Naomba nisinukuliwe vibaya, hapa tuko tu katika kukumbushana kwani naona tumeanza kujisahau. Kufanya yale tuliyokubalana ni bora kwa maelewano katika jamii.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection