Unaeokota Naye Kuni Ndiye Unaeota Naye Moto.

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kuni ni mojawapo ya nishati inayotumika sana barani Afrika. Kwa kawaida, kuni zinaokotwa au kukusanywa kutoka kwenye miti porini.

Msemo huu unaweza kuwa na maana mbali mbali kwenye jamii zetu. Maana mojawapo inaweza kuwa ya mtu ambaye mmeanza naye maisha ya chini kabisa mpaka mkafikia maisha ya mafanikio mkiwa wote. Mtu huyo ndiye ambaye mtakula naye mafanikio.

Wapo watu wanaoanza biashara pamoja, mfano biashara ya magari ya aina yoyote. Watu hawa wanaendelea mpaka wanakuwa na magari mengi hadi wanaamua wagawane ili kila mmoja aweze kuendesha biashara yake kutokana na mafanikio waliyopata. Huu unaweza kuwa mfano wa mtu anayeokota kuni na wewe, huyo ndiye tunasema utaota naye moto.

Swali ni je, tuko tayari kuanzia maisha yetu chini na rafiki zetu, jamii zetu, ndugu zetu? Au tunakuwa tayari kudhulumiana hata kabla ya kufikia kuota moto pamoja? Hili ni swali zuri na la msingi ambalo yatupasa tujiulize. Kimsingi, binadamu maisha yetu lazima yawe yale ya kushirikiana na kusaidiana kwa kila jambo. Huo ndio unatakiwa kuwa utaratibu wa maisha yetu ambao tunapaswa kuwa nao. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Haki Ya Mtu Hailiki!

Next
Next

Kipimo Chako Siku Zote Ni Ufanisi.