Haki Ya Mtu Hailiki!

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Haki ni kitu halali kinyume cha batili. Mwenye kutoa haki ni Mwenyezi Mungu peke yake, Yeye akisema amesema huwa hakuna wa kumpinga. Mwenyezi Mungu anaweza kuwatumia watu wakupatie haki yako. Mara nyingi tunaona na kuthibitisha ukweli wa usemi huu wa haki ya mtu hailiki bali hucheleweshwa tu.
Hebu na tuchukue mfano wa kiongozi wa Afrika ya Kusini, Neslson Mandela. Tunaona jinsi alivyofungwa jela miaka 27 kwa kutetea haki za watu wa taifa lake. Tunaona jinsi alivyofunguliwa baadaye na akaweza kuitawala nchi yake, Afrika Kusini. Hapo tunaona jinsi haki yake alivyoipata, haikuliwa, bali ilicheleweshwa tu.
Kama binadamu, tunatakiwa kuwa wavumilivu. Hivyo wewe unayengoja kupandishwa cheo kazini kwako yakupasa uwe mvumilivu. Wewe ambaye umekuwa ukifanya biashara ya ufugaji kwa muda mrefu sana, na wewe ambaye umekuwa ukilima kwa bidii sana bila kuona mafanikio yoyote, tambua kuwa haki yako iko njiani, inakuja, cha msingi unatakiwa kuwa na subira, usikate tamaa. Daima kumbuka kuwa, haki ya mtu huwa hailiwi. Mtoa haki anapoona bidii yako atakupatia haki yako. Wahenga walinena, subira yavuta heri.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection