Mlibua Nchi Ni Mwananchi.

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mlimbua nchi ni mtu ambaye anaifahamu sana nchi yake. Kwa
maneno ya sasa huyu mlimbua nchi tunasema mhujumu wa nchi yaani anaisema vibaya nchi yake; anatoa siri za nchi yake, anaiweka nchi yake katika hali ya hatari kwa namna yeyote anayotaka yeye.

Mambo kama haya yanaweza kutokea kwenye ofisi ambayo mtu anafanya kazi. Anaweza kuwa amekaa kwenye ofisi hiyo kwa muda wa zaidi ya miaka mitano. Sasa endapo baadaye ajira yake inasitishwa, bila kujali muda liohudumu, ataanza kutoa siri za hapo mahala. Anasahau manufaa aliyopata akiwa hapo kazini.

Mambo kama haya ya kulimbua yanaweza kutokea mahali popote, pamoja na kwenye misikiti na makanisa ambako watu huenda kusali. Mara nyingi watu hawa hufanya hivyo baada ya kushindwa kuwa waumini wazuri. Kutokana na hali hiyo, huanza kutoa siri za mahali hapo na kutoa kashifa pia.

Hivyo wananchi wenzangu, wanaamini wenzangu, na tulioko maofisini, tusiwe watu wa kutoa siri bali tuhifadhi madhaifu tuyaonayo na ikibidi tueleze madhaifu hayo kwa wahusika ili waweze kujirekebisha au kusahihisha maovu yao. Kubwata bwata ovyo hakuleti tija yoyote katika maisha ya binadamu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Ujuzi Hauzeeki!

Next
Next

Haki Ya Mtu Hailiki!