Ujuzi Hauzeeki!

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Ujuzi ni ufundi au kipaji cha kufanya vitu ili kukuletea faida au kukuingizia kipato. Ujuzi unaweza kupatikana kupitia mafunzo. Hali kadhalika, ujuzi unaweza kutokana na kipaji cha kuzaliwa nacho mtu ambacho kinamuwezesha kufanya vitu vya pekee na vizuri vinavyoweza kununuliwa na watu na hivyo kukupatia kipato.
Kwa kawaida, ujuzi hauzeeki. Kadri mtu anavyozidi kuufanyia kazi ujuzi huo ndivyo unavyoongezeka. Hata mtu akianza kuzeeka, ndivyo ujuzi huo unavyozidi kuendelea kukua zaidi na zaidi.
Tunawaasa vijana hasa wale ambao hamna ajira na ambao hamna vipaji vya kuwawezesha kupata kipato kuwa watafute namna ya kwenda kusomea ujuzi wanaoupenda ili wakishafuzu, waweze kujiajiri wenyewe na hivyo kujiingizia kipato na hatimaye kuwa na uwezo wa kuendesha maisha na kutunza familia zao.
Ujuzi hauzeeki kwa vile kadri unavyojikita katika ujuzi wa aina fulani kwa muda mrefu ndivyo unavyozidi kuongezaka na kuwa bora zaidi. Ujuzi ni ajira tosha kwa vijana, hivyo msihangaike kungojea kuajiriwa. Tunasisitiza kwa vijana umuhimu wa kupata ujuzi ili muweze kujiajiri wenyewe. Mkifanya hivyo mtaepukana na msongo wa mawazo ambao umekuwa ni tishio kwa vijana wengi hapa nchini. Hima vijana, Pam bane i na maisha yenu kwani maendeleo yapo mikononi mwenu, msingoje kuletewa, hususani, pale yanapochelewa kukufikia.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection