Tabia Zako Zinaweza Kukufanya Upoteze Fedha Zako!

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Tabia zako zinaweza kukufanya upoteze fedha zako, ziwe nyingi au chache.
Hali hiyo ya kupoteza fedha inapokithiri unaweza kuamini kuwa ni mchezo wa ‘chuma ulete’ na unaweza kujikuta unakwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta suluhu. Mwisho wa siku unakuja kuona kuwa kumbe ni tabia zako mbaya usizozitambua ambazo zimekufikisha hapo.
Baadhi ya tabia hizo ni pamoja na matumizi ya pesa zaidi ya kipato chako, tamaa ya vitu vya gharama kuzidi kipato chako na kununua vitu hovyo hovyo bila kuwa na mpangilio ili mradi tu una pesa mfukoni. Tabia nyingine ni ile ya kupenda kukopa kopa bila malengo maalumu kama vile kuwekeza kwa faida ya baadaye.
Tabia hizo zinaweza kukufanya uwe maskini, mdaiwa na hata kuishi kwa hofu siku zote za maisha yako. Tunachotakiwa kufanya ni kuweka kipaumbele kwa mahitaji muhimu. Hali kadhalika, yatupasa kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha zetu. Pia tunatakiwa kuwa na mpangilio mzuri wa fedha zetu bila kusahau kuweka kumbukumbu za matumizi ya pesa zetu.
Ukizingatia yote hayo, utaepuka kuingia kwenye matatizo makubwa ambayo yatakusononesha na hatimaye ukaishia kupata sonona ambayo itakusumbua na kukufanya usimame kufanya shughuli zako za kimaendeleo.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection