Mtaka Cha Uvunguni, Shart Ainame!

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Hakuna mafanikio yatakayokujia ukiwa umekaa tu ma kubweteka huku ulingojea msaada kutoka kwa ndugu, jamaa na marafik. Mafanikio yanahitaji kujishughulisha ili uweze kuhimili changamoto zinazojitokeza. Maana kila unachokifikiria lazima kitakuwa na pingamizi au maswali ambayo ni hasi na magumu.
Usipopambanua hayo maswali yanayokuja, ujue lile jambo ambalo unalitegemea lipate majibu halitajibika. Mara nyingi majibu ya suala lolote yanakuwa yamejificha. Ili ulipate lazima ukubaliane na zile changamoto kuwa zipo, hapo ndipo utaweza kufikia hatma yako. Kama ambavyo kilichopo chini ya uvungu wa kitanda huwezi kukiona mpaka uiname ndivyo ilivyo katika mmaisha. Juhudi zako za kapambana na changamoto, ndizo zitakuletea mafanikio.
Hata vitabu vya Dini navyo vinasema ‘asiye fanya kazi na asile’. Hata bila maonyp hayo kwenye vitabu vya dini, mtu asiyefanya kazi, atakuwa hajielewi. Hapo ndipo hata afya yako ya akili itaanza kupitia vikwazo na kuanza kutetereka. Kumbuka, afya yako ya akili itakuwa vizuri na imara pale tu mahitaji ya muhimu, yako na ya familia yanapatikana. Bila hivyo utaishi kwa matatizo, wasiwasi na mahangaiko tele.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection