Wema Sio Deni, Usisubiri Kulipwa.

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kuna tabia iliyojengeka katika jamii ya kufikiria kuwa unayemfanyia wema ni lazima akulipe. Kuna wale ambao wamesomesha watoto, ndugu na jamaa wengi tu kwa kutegemea kuwa watarudishiwa fadhila kwa wema walioufanya. Kwa bahati mbaya, watu hawa hungojea weee na kukuta hakuna majibu wala fadhila yoyote inayokuja. Hizo huwa ni hisia au mategemeo ya walio wengi.

Lakini ukweli ni kwamba, katika wengi uliowasaidia na kuwafanyia wema sio lazima wakurudishie fadhila. Anaweza akatokea mmoja tu ambaye atarudisha fadhila. Hata Yesu aliwauliza watu kwa kusema: “Je sikuwahudumia kumi lakini aliyerudi ni mmoja tu”. Tujifunze kitu hapa.

Tatizo kubwa tulilo nalo ni kutaka kutangaza yale tuliyowafanyia watu yajulikane kwa kila mtu . Unataka watu wakuone kuwa wewe ni mwema. Kuna usemi usemao, “Tenda Wema Nenda zako, Usingoje Shukurani”. Haina maana kuwa kila siku wewe ndio utakuwa wa kusaidia tu, hata nawe utahitaji msaada kutoka kwa wenzio. Binadamu tunategemeana hata kwa kidogo alichokuwa nacho mwenzio.

Yatupasa tumheshimu kila mtu kwa sababu kila mtu ni wa muhimu kwako kwa wakati usioujua. Kumbuka, wema sio deni na kamwe usisubiri malipo. Yatupasa tuiache tabia hiyo mbaya, uliyemsaidia wema, wewe nenda zako na wala usingoje shukurani. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Heshimu Muda Nao Utakuheshimu.

Next
Next

Mtaka Cha Uvunguni, Shart Ainame!