Heshimu Muda Nao Utakuheshimu.

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Muda ni kitu cha thamani sana ambacho tumepewa bure na Mwenyenzi Mungu. Kila mtu amepewa bila upendeleo. Kwa kawaida, ukiuheshimu na kuujali muda, nao utakulipa kwani utaona matokeo tatakayokuja kuwa ni mazuri.

Hapa duniani watu wengi waliojali, walioheshimu na kutunza muda vizuri wamefanikiwa sana kimaisha. Hata hivyo, heshima ya mtu yeyote hutokana na anavyojali na kuheshimu muda wake na muda wa wengine pia.

Ukichezea au ukipoteza muda wako katika maisha, ni sawa na umepoteza dira ya maisha yako, kwani muda haurudi nyuma wala haumsubiri mtu yeyote.

Yatupasa tujifunze kuwa tunatakiwa kuujali, kuuheshimu na kuutunza muda wetu ambao ni wa thamani sana kwa maisha yetu sisi wanadamu. Kama tunataka kupata matokeo mazuri katika maisha, hatuna budi kukubaliana na ushauri huu. Pamoja na yote hayo tusisahau kumshukuru Mungu kwani ndiye aliyetupa huo muda. Bila Yeye hakuna kinachowezekana.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Angalia Namna Ya Kuongea Kwako.

Next
Next

Wema Sio Deni, Usisubiri Kulipwa.