Angalia Namna Ya Kuongea Kwako.

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Lugha inaweza kubadilisha hali ya hewa katika mambo mengi ufanyayo. Matumizi ya lugha yanaweza kubadilisha maisha yako na jamii inayokuzunguka. Maisha ya ndoa yako, kama wewe ni mwanandoa, yanaweza kubadilika pia. Malezi ya watoto yanaweza yakabadilika katika familia zetu kutokana na luga tunazotumia. Lugha kali kwa watoto huwaogopesha kiasi hata kukosa amani na wazazi. Watoto wakiishi kwa woga, wanaweza hata kuingia kwenye makundi mabaya ili kupata faraja. Nyumbani watapaogopa, hawatapenda kukaa na hasa pale mzazi mwenye lugha ya kukera akiwepo. Watoto wakiishi katika mazingira hayo, wanaweza kujifunza mambo yasiyofaa. Wahenga walisema, samaki mkunje angali mbichi, akikauka hakunjiki.

Lugha nzuri itawapa watoto malezi bora.
Lugha yako inaweza kukupa mafanikio katika maeneo mengi. Mathalani, ukiwa kwenye biashara, lugha yako ikiwa nzuri, itawavutia wateja na hivyo kuwafanya wapende huduma uzitoazo. Lugha unayotumia itafungua milango hata pale palipokuwa pagumu. Yakupasa uwe makini kila siku. Maneno yako yawe machache ili uweze kuhudumia wateja wako kwa haraka na hivyo kuleta ufanisi katika biashara yako na hatimaye uweze kufikia malengo yako.

 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Shujaa Haangamizwi Na Mwoga!

Next
Next

Heshimu Muda Nao Utakuheshimu.