Shujaa Haangamizwi Na Mwoga!

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Shujaa ni yule mtu ambaye haogopi kuthubutu katika jambo lolote. Hata kama mahali ni pagumu, atajitahidi ili apite au atimize lengo alilokusudia. Mara nyingi mbele yake woga unakuwa haupo. Shujaa huwa anaangalia malengo yake kwa makini.

Mara nyingi shujaa huwa hayuko tayari kumshirikisha mtu mwingine katika maamuzi yake. Kwa maneno mengine, shujaa huwa ni mtu aliye na ujasiri wa hali ya juu. Yeye huwa haogopi chochote. Uthubutu ndiyo ndiyo nyenzo ya maisha yake.

Mara nyingi mtu mwoga huwa ana ile hali ya kukata tamaa. Mtu kama huyu hushindwa kufikia malengo yake. Watu wa aina hii huwa wana tabia ya kupenda kumtoa mtu kwenye misimamo yake. Pale ambapo mtu hana msimamo, huweza kuingizwa kwenye misimamo ya wavivu ambayo itakuwa haina tija katika maisha yako

Ukiwa mwoga wa kuthubutu, utajikuta umeingizwa kwenye mifumo yao ya uoga. Mwoga huwa ni mjanja maana kazi yake kubwa ni kuwatafuta watu wa kufanana naye. Kutokana na mazingira kama haya ya kudanganyana, tunatakiwa kuwa makini na kila tufanyacho. Tufanye kwa ushujaa, uangalifu na ujasiri ili tuweze kuwashinda watu waoga ambao kazi yao ni kuwatoa watu kwenye reli.

 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Raha Jipe Mwenyewe!

Next
Next

Angalia Namna Ya Kuongea Kwako.