Raha Jipe Mwenyewe!

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Furaha ni hali ya kuishi kwa amani na utulivu bila msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo ni hali ya kuwa na stress mbalimbali zinazokusumbua katika maisha, kama vile huzuni, kukosa amani na raha, kuwa na mawazo mengi n.k.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yatakufanya uwe na furaha. Baadhi ya mambo hayo ni:

  • Kujiamini ambako hukufanya uwe na amani na uhakika wa unachokitarajia.
  • ⁠Kujiheshimu huwafanya na wengine waige tabia zako ambazo huziona kuwa ni nzuri.

Jambo jingine kubwa litakalokufanya uwe na furaha ni kusamehe watu ambao wamekukosea. Kusamehe huleta amani katika maisha ya mwanadamu. Usigpmbane na watu, usiwe na kinyongo na uwe na kipimo cha maneno, wakati mwingine, jifunze hata kukaa kimya.

Kitu kingine cha msingi pia ni kujipenda. Yakupasa uwe mtanashati, usijidharau wala usijishushe viwango. Daima jitamkie mambo mazuri yatakatokupa furaha. Jifunze kurejea mambo mazuri yaliyopita ili kupata faraja.

Kila uchwapo, penda kujifunza kitu kipya. Wakati wote kuwa na tabia ya kutabasamu
kwani furaha ni tiba ya moyo. Panga malengo yako kwani ni dira ya kesho yako. Usisahau kula vizuri. Ridhisha moyo wako kwa kula kile unachokipenda ila kula kinachohitajika mwilini mwako.

Kumbuka kumshukuru Mungu kwani yeye ndiye
mpaji wa vyote.
Ukizingatia hayo yote utakuwa na maisha yenye furaha na amani tele. Wahenga walinena raha jipe mwenyewe, usisubiri uletewe.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Mwana Mtukutu Hali Ugali Mkavu!

Next
Next

Shujaa Haangamizwi Na Mwoga!