Mwana Mtukutu Hali Ugali Mkavu!

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Wazazi wengi tunabarikiwa na Mungu kupata watoto na ndio furaha kubwa katika ndoa zilizo nyingi. Hata hivyo, wapo wanandoa wengine ambao hawajabarikiwa kupata watoto. Yote ni kazi ya Mungu.
Baada ya baraka hii ya ndoa wazazi huingia katika malezi. Mzigo wa malezi huwa siyo lelemama kwa wazazi wengi. Mara zote wazazi wanaeelekeza watoto wao wafanye mambo ambayo ni mazuri. Pale watoto wasipotii, wazazi huumia sana. Ukweli unaonyesha kwamba kwa sasa watoto wengi wanapenda kulala muda mrefu bila kufanya kazi.
Wengi wa watoto hawa, wawe wa kiume ama wa kike hawawezi kufanya kazi za nyumbani. Ukitaja kazi za shambani ndiyo kabisa hawawezi. Watoto kama hao wasipozingatia malezi waliyopata kutoka kwa wazazi wao, watakuja kuingia kwenye kundi la watoto watukutu
Mtoto mtukutu hutafuta chakula mahali popote. Endapo atatumwa kwenda kununua chakula, hata kama hajapewa kibali cha kula, yeye hujichukulia mamlaka ya kukila chakula hicho. Licha ya hivyo, akikuta ugali mahali, hata kama hajakuta kitoweo au mboga, atatafuta kila mahali ili aweze kula na huo ugali.
Hali kadhalika, mtoto mtukutu ni mdadisi sana hivyo hawezi kula ugali mkavu. Atahangaika wee na ataomba hata kwa jirani kwa kutumia mbinu za uongo.
Mtoto mtukutu huwa ana sifa ya kuchukiwa na familia na hata majirani kwa sababu ya ukaidi wake. Tunaaswa kutokuwa kama mwana mtukutu. Utukutu una hasara nyingi ambazo zinaweza kutukuta huko mbeleni.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection