Endelea Kujaribu.

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Ni kawaida kabisa kwa mtoto anapotaka kuanza kusimama kushika na kuegemea kila kitu ili kimsaidie asimame. Wakati mwingine anaweza hata kuegemea vitu vya hatari, kama vile chupa ya chai, jiko la moto na vingine vingi tu vinavyokuwa karibu yake. Kwa ujumla, anaweza kushika kitu chochote ambacho kinaweza kuwa ni cha hatari ili mradi tu asimame.

Mara nyingi katika hatua hii ya mtoto kutaka kusimama huwa ndio kipindi ambacho anaharibu vitu na kuvunja vitu vingi. Mara nyingi, hii huweza kusababisha hasara kubwa kwenye familia. Baada ya mihangaiko mingi ya kuanguka, kuumia na kusimama, hatimaye mtoto hutoka katika hatua hiyo na kuweza kusimama bila kuegemea chochote. Hapo tunaweza kusema, mtoto ameanza kukomaa.

Huo ndio ukweli pia katika maisha yetu sisi wanadamu. Pale unapoanza hatua za kusimama mwenyewe kutengeneza maisha yako, utashika hiki kinashindikana, utashika kile nacho pia kinaharibika. Utahangaika kufanya vingine, napo unajikuta kwenye hasara na kuingia kwenye mambo mengi, na mengine yakuumiza pia. Hali kadhalika, unaweza kuumiza hata wengine. Hapa tunaona pilika pilika zile zile kama za mtoto mchanga anapoanza kutaka kusimama mwenyewe.

Nawe pia usikate tamaa endelea kufanya, endelea kujaribu tena na tena kwa umakini mkubwa hatimaye, utasimama kabisa. Maisha ndivyo yalivyo, yatupasa tupambane hadi tusimame tuwe imara.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Usiige Wala Kukata Tamaa Ungali Hai.

Next
Next

Donda La Kichwa Mkaguzi Mkono!