Usiige Wala Kukata Tamaa Ungali Hai.

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Mara nyingi sisi,
binadamu tunakuwa na tabia ya kukata tamaa ya kuendelea na maisha mara tunapokwama kidogo. Huwa tunasahau kuwa mafanikio hayaji ghafla na kwamba nyuma ya kila fanikio, lazima kuna maumivu makali. Hata dhahabu ili iwe dhahabu bomba ni lazima kupitia kwenye moto mkali sana. Hivyo hatutakiwi kukata tamaa katika hali yoyote ile tunayopitia, bali tunatakiwa kuongeza bidii. Aidha, bidii ya mtu yeyote tangu awali ndiyo mafanikio yake ya baadaye.
Hata hivyo si vyema kutamani maisha ya mtu mwingine kwani hatujui walifanya nini hadi wakafanikiwa kimaisha. Pia siyo kila mtu unayemwona akitembea haraka haraka anawahi ahadi mahali fulani; la hasha! Wengine wana matumbo ya kuharisha au shida nyingine nyingine zilizo nyeti na za msingi.
Hivyo hatutakiwi kuiga kila jambo tulionalo. Pia, tusipende kujilinganisha na watu wengine kwa hali na mali. Tunachotakiwa kufanya ni kujiamini kwa uwezo tulio nao kwani huo ndio mtaji wetu.
Kutokana na simulizi hii tunajifunza umuhimu wa kujithamini. Kamwe tusipende kujidharau. Kila mtu ana thamani kubwa, ni lazima tutambue hilo.
Yatupasa tuwe na malengo na bidii na kisha tunatakiwa tusonge mbele. Kwa kuzingatia na kutekeleza hayo bila shaka yoyote tutatoboa kimaisha.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection