Hujafa Hujaumbika.

Avelina Hokororo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika maisha tunatambua wazi kuwa Mungu ametuumba na tumekamilika, hata kama hujakamililika katika viungo vingine lakini upo vizuri.
Sasa kuna wengine wana tabia ya kuwacheka wenye vilema. Hujui kilema hicho kazaliwa nacho au kakipatia ukubwani.
Kumbuka kwamba Mwenyezi Mungu kila siku anakukarabati yaani anakuumba wewe mpaka utakapoondoka hapa duniani na kurejea kwake.

Nafikiri wengi tumeishapata vilema tayari tumekwisha kuzaliwa, na pengine baada ya kukua na hata uzeeni.

Katika maisha kuna changamoto mbalimbali zinazoweza kumpata mwanadamu, mathalani kupata ajali ambazo zinaweza kukufanya upoteze viungo vyako vya mwilini kama miguu au mikono. Unaweza kuzaliwa ukiwa na meno, na hivyo ndivyo Mungu alivyokuumba. Kwa kawaida, utang’oa meno ya utotoni na halafu yakaota meno mengine mazuri.

Unaweza kuzaliwa ukiwa na mdomo ambao una umbile zuri tu wakati unacheka. Lakini kwa kuwa Mungu anaendelea kukuumba kila siku unaweza ukajikuta kila mwaka unang'oa na kuziba meno. Na hatimaye, hadi unafikia uzeeni unajikuta una jino moja au huna kabisa.

Wewe unapomcheka huyo mwenye ulemavu, kumbuka Mungu yupo kazini. Unaweza ukapata ajali, macho yakaondolewa yote mawili, au mikono na miguu yote, ikakatika.

Kutokana na simulizi hii, tunaaswa tusiwacheke watu wenye ulemavu wa aina yoyote. Kumbuka, Mungu bado anakuumba wewe hadi siku utakapoondoka hapa duniani. Cha msingi hapa ni kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Hii inakuhusu wewe uliye mzima mpaka sasa. Endelea kumuomba Mungu wako ili akuepushe na majanga. Na sisi tuliokuwa na vilema, yatupasa tumshukuru Mungu aendelee kututunza mpaka tutakaporudi kwake.

Kabla ya kufa, usijisifie na kusema kuwa wewe umeumbika na kuwa wewe ni mzuri. Safari yako ya mwisho haijafika, hujui litakalokupata huko mbeleni. Wewe hudhibiti maisha yako hata kidogo. Daima inakupasa ukumbuke hilo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Mafanikio Yanahitaji Kufahamu Na Kukipenda Kile Unachokifanya.

Next
Next

Usiige Wala Kukata Tamaa Ungali Hai.