Mafanikio Yanahitaji Kufahamu Na Kukipenda Kile Unachokifanya.

Simulizi
Hapa duniani yako mambo mengi sana tusiyoyajua. Lakini ili tufanikiwe katika jambo fulani lazima tuwe na ufahamu na hilo jambo.
Shuhuda nyingi zinaonyesha kuwa ili kufanikiwa katika jambo ni lazima moyo wako na akili yako vilipende jambo lenyewe. Hata kwenye biashara, tunashauriwa tufanye biashara ambayo mioyo yetu imeridhika na kufurahiwa nayo. Ukilazimisha kufanya biashara ili mradi tu ufanye, kamwe hautafanikiwa.
Kwa maana hiyo basi tunashauriwa tusifanye tu jambo kwa sababu hatuna jambo jingine la kufanya. Ni lazima mioyo na nafsi zetu ziridhie kwanza kufanya hilo jambo ili tuweze kufanikiwa.
Kwa kadri ya uelewa wako na jambo lenyewe unalotaka kulifanya, ndivyo utakavyofanikiwa na kustawi.
Kiuhalisia, tumeona kuwa watu wenye ufahamu si wengi sana. Pengine huenda hii ndio sababu ya kuwa na watu wachache ambao wamefanikiwa na kustawi.
Ukweli ni kwamba usitawi na mafanikio yako uttatokana na kile unachokifahamu.
Kupitia hicho unacho kifahamu ndicho kitakachokuwezesha kufikia usitawi na kupata mafanikio yako.by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection