Ukiambiwa Ubaya Wa Mtu, Tafuta Uzuri Wake.

Simulizi
by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Binadamu tuna tabia moja ya ajabu sana. Mara nyingi tukiambiwa kuwa fulani ni mbaya tunaamini mia kwa mia na kuufanya ubaya wake kuwa ni fimbo ya kumchapia kila uchao. Kila jambo atakalotenda linakuwa ni baya tu kwa jamii inayomzunguka. Ubaya wake unakuwa umekwisha tia mhuri kwenye mioyo ya watu kiasi kwamba hata akipita mahali popote pale atakuwa ni wa kunyooshea vidole tu.
Ni mara nyingi tunasikia watu wakisema ”Hakuna binadamu aliyekamilika”. Tunaona kwamba kukosa huo ukamilifu kunatufanya tumuone huyo jamaa kuwa hana faida yeyote kwenye jamii yale. Ukweli ni kwamba siyo kweli. Ukiwa na muda na kufanya uchunguzi unaweza ukapata ukweli kuhusu mtu huyo. Pamoja na kwamba amefanya mabaya mengi, ana mambo mazuri mengi pia ambao hamuyajui. Kutokana na mabaya yake, jamii huyadharau mema yake yote na kuyaona kama vile hayana thamani tena.
Nimewahi kushuhudia tatizo ambalo lilitokea kwenye mtaa wetu. Jamaa huyo huyo waliyemwona mbaya alijitoa sana kwenye msiba uliotokea hapo mtaani hadi watu wakashangaa. Alijitolea vitu vingi kweli pale msibani kuliko mtu mwingine yeyote. Pamoja na kwamba walimbeza sana waliishia kuvitumia vitu alivyovileta. Hii ulifanya kidomodomo chote kiishie hapo.
Kutokana na simulizi hii, tunajifunza kuwa mtu mwenye ubaya ana uzuri wake pia. Tusipende kuwahukumu na kuwatendea mabaya watu ambao wanaongelewa kwa ubaya. Watu hao hao tunaowaona kuwa ni wabaya, wanaweza wakaja kutusaidia huko mbele ya safari ya maisha yetu. Kila mtu ni wa muhimu katika dunia hii. Yatupasa tuheshimiane na kuthaminiana kwani kila mtu ana jema la kutoa kwa wenzie.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection