Anachoweza Kukufanyia Jogoo Ni Kukupigia Kelele Na Sio Kukutoa Kitandani.

Simulizi
Maisha yetu yanatawaliwa na mambo mengi sana. Mengi tuyafanyayo yanatokana na kufundishwa au kuelekezwa. Katika mambo mengi tunayofundishwa kama tungekuwa tunayatendea kazi tungekuwa mbali sana. Kumbuka kuna mangapi tumesoma ambayo ni ya msingi lakini hatuyafanyii kazi. Huu ndio ukweli wenyewe.
Tukirudi kwenye tewwy, sisi wanasihi tumeelekezwa mengi ambayo tunaweza kuyatumia katika maisha yetu. Baadhi ya vitu tulivyojifunza ni kutengeneza sabuni na kutunga shanga.
Siku hizi kuna mtindo wa kuvaa shanga mikononi kwa wakina mama wengi. Kwa hali hiyo tewwy tunaweza kuifananisha na jogoo yeye anakupigia kelele lakini ni hiyari yako kuamuka au kuendelea kulala. Kazi yake ameifanya kwa nafasi yake. Tujitahidi kuyafanyia kazi yale tunayofundishwa.
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection