Donda La Kichwa Mkaguzi Mkono!

Simulizi
Ni ukweli usiopingika kuwa kila binadamu lazima atakuwa na mtu au watu wa karibu ambao huwa ni tegemeo lake katika mambo mengi ayatendayo, hususani wakati wa shida ama wakati wa raha. Wako watu ambao wanaweza kuwa karibu zaidi kiasi kwamba kunakuwa hakuna jambo unaloweza
kulifanya bila wao kujua au kuchangia mawazo.
Kutokana na hali hiyo, pale inapotokea kuwa umeharibikiwa, wa kwanza atakayeweza kueneza habari hizo ni yule wa karibu yako. Kama ni ushahidi yeye ndiye anayeweza kukukandamiza vizuri.
Sambamba na usemi huu ni ule usemao kuwa ‘Unaweza kufaidika na yule unayemuita adui pia unaweza kuhuzunika na yule unayemuita rafiki’. Adui yako atakuogopa na pia hataweza kukukaribia maana hamko karibu. Aliye karibu yako ndiye atakayekuumiza. Hii ndio maana halisi ya usemi huu wa donda la kichwa mkaguzi mkono. Mkono ndio unaofika kichwani kwa mtu. Hivyo yatupasa
kuwa makini na mtu aliye karibu yetu. Anaweza akatumaliza kiurahisi sana.
Hali kadhalika, wahenga walisema ‘Kikulacho ki nguoni mwako’ wakiwa na maana hiyo hiyo na hivyo kutia mkazo zaidi wa hayo yaliyoelezwa hapo juu.
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection