Wajibika Na Maisha Yako

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Hapa duniani, kila mtu anatakiwa kupambania maisha yake. Unaposimamia na kudhibiti shughuli zako mwenyewe utaridhika, utapata amani, furaha na faida.
Lakini siku zote hazifanani, wakati mwingine mambo huenda kombo, hivyo unatakiwa kupokea hiyo hali na kuitumia kama fursa ya kujirekebisha, kujifunza zaidi na kuendelea kuwajibika.
Endapo mambo yako hayaendi vizuri, yakupasa uridhike na hiyo hali. Kamwe usipende kuwalaumu watu wengine au kuwachukia na kuwawekea kinyongo na hata kuwaonea wivu. Hutakiwi kumlalamikia mtu yeyote, na wala wazazi, ndugu, marafiki au ofisi uliyopita kwamba wao ndio wamechangia maisha yako kuwa ya hovyo. Jitafiti kwanza wewe mwenyewe, ni wapi ulipokosea ili uweze kurekebisha na kuweza kusonga mbele.
Huenda wewe ndiye uliyefanya makosa tokea awali. Kwa mfano, pengine ulikuwa mtoro shuleni, hilo nalo huwa ni tatizo kubwa kwa walio wengi. Labda ulikuwa na utovu wa adabu na hesima. Huenda ulikuwa unajihusisha na makundi mabaya au ulikuwa huwasikilizi wazazi wako.
Unachotakiwa kufanya ni kujitambua, kujirekebisha na kujua kuwa maisha yako ni yako na siyo ya mtu mwingine hivyo ni muhimu kuwajibika kwa kuyasimamia maisha yako wewe mwenyewe. Cha msingi zaidi ni kutambua kuwa wewe ndiye mtawala mkuu wa maisha yako na si vinginevyo. Unatakiwa kuwajibika, na hii ni lazima kwa kila mtu, na siyo hiari. Daima tukumbuke wosia huu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection