Usilaumu Kimbunga, Tunza Mkeo.

Simulizi
by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Siyo jambo geni kwenye jamii zetu kusikia kuwa jukumu na wajibu wa msingi wa kila mwanaume ni kumtunza mke wake kwa kumpatia mahitaji yake ya msingi. Lakini maisha yamebadilika na hivyo kufanya majukumu yabadilike pia. Hii ni kutokana na hali ngumu ya maisha. Kwa kiasi kikubwa, wanawake wengi wamekuwa wakilalamikia wanaume kusahau majukumu yao. Hii imesababisha ndoa nyingi kuvunjika.
Hali kadhalika, kumekuwa na tabia ya mabinti wengi kupenda kuolewa kwa malengo fulani fulani ambayo hayana uvumilivu ndani yake. Kuna wengine wakishaona fulani kaolewa, nao watatafuta kila mbinu na kulazimisha ndoa ili mradi tuu nao waolewe bila kujua hali halisi aliyokuwa nayo huyo bwana. Tumeshuhudia kuwa kwa muda mfupi, mambo yakienda vizuri pale mume asipoonyesha ukweli wa hali yake. Lakini baada ya hapo mwanaume itampasa aonyeshe uhalisia wake. Ule uwezo wa kutimiza mahitaji ya mke wake unayeyuka.
Hapo ndipo malumbano huanza. Wawili hao huanzisha vurugu na hali ya kutoelewana. Makelele yanakuwa ni ya kila siku, hayaishi. Mwisho wake mke anaamua kuachia ngazi na kuanza kutafuta maisha ama mchepuko mwingine ili mradi tu aweze kupata huduma.
Haya mambo yanaendelea sana kwenye jamii zetu za kitanzania. Ndoa nyigi huvunjika na ni sababu kubwa kwa mabinti zetu hukosa uvumilivu kwa ajili ya kuendekeza tamaa.
Kutokana na somo hili tunajifunza kuwa mwanamke ni kama bati, usipoligongea misumari imara utalikuta kwa jirani. Vilevile mabinti zetu wanaaswa kuwa wavumilivu. Inawabidi waache tamaa ambazo hazina msingi. Na wajue kuwa kuvumiliana kunaleta baraka kwenye familia na hata kuinua kiwa
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection









