Usipime Mafanikio Yako Na wale Walio Kuzidi.

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

Mipango ya watu wengi huwa ni ya kuleta mafanikio na sio vinginevyo. Unapoweka mipango yako unaweka na mikakati ya jinsi ya kutekeleza hiyo mipango. Mikakati hiyo itatakiwa iwe na uwezeshaji, inawezekana kifedha au kimawazo. Kama ni kifedha, unaweza kutumia njia ya kukopa au vinginevyo. Kama ni kimawazo, utahitaji kupata mawazo kutoka kwa watu mbalimbali, watu wenye busara na uungwana.

Hapo ndipo unapotakiwa kuwa makini ili uweze kupata ushauri wa kujenga. Kuna baadhi ya watu huwa wana ushauri wa kudidimiza na sio wa kujenga. Mara nyingi watu hao huwa ni wale ambao wamekuzidi kiuwezo. Sio wote ambao wangependa ufike pale walipo wao. Kwa hiyo inakupasa uangalie ni nani na ni yupi anayeweza kuwa wa msaada kwako. Ndio maana inashauriwa awe mtu mwenye busara na uungwana, mtu mwenye moyo wa kuwajali binadamu wenzie. La sivyo, ukikosa watu wa aina hii, itakupasa kupambana mwenyewe kwa kadri utakavyojaliwa.

Kila mwanadamu yampasa awe na msimamo. Yampasa asimamie kile ambacho alikiwaza yeye mwenyewe. Hii ni kwa sababu watu walio wengi, kazi yao ni kurudisha nyuma wenzao na mwisho wake wanaishia kukusema na kukucheka. Kwa hakika, binadamu ni kiumbe wa ajabu. Hatabiriki kabisa. Kuwa mwangalifu.

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Usilaumu Kimbunga, Tunza Mkeo.

Next
Next

Ujinga Mzigo!