Ujinga Mzigo!

Simulizi
by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Tujikumbushe kwanza hilo neno ujinga ni nini. Ujinga ni ile hali ya mtu asiyejitambua au kukosa ufahamu wa kufanya jambo lolote lenye manufaa au faida kwa kutumia akili zake mwrnyewe. Bila shaka tunajionea wenyewe jinsi Serikali yetu inavyojitahidi kutoa elimu bure kwa watoto wetu na hata kutoa mikopo kwa vijana wetu wanaoingia Chuo Kikuu. Lengo kuu la kufanya hivyo kuwapa elimu ili kufuta ujinga. Taifa linatakiwa liwe na watu wenye maarifa, uelewa na uwezo wa kujitambua wa kufanya shughuli za maendeleo ya taifa lao wakiwa na uelewa zaidi.
Kuwa na nchi ambayo watu wake hawana elimu ni mzigo mkubwa kwa taifa. Ndio maana tunasema ujinga mzigo. Mtu akiwa mjinga hakuna atakaye mthamini, badala yake utakuta watu mitaani wakimzungumzia vibaya na kumuona hana thamani yeyote kwenye jamii. Hii ina maana kuwa atatwishwa kila aina ya sifa mbaya kiasi kwamba atashindwa kubeba huo mzigo wa sifa mbaya.
Kwa somo hili tunajifunza kuwa elimu ni muhimu katika maendeleo yetu na maendeleo ya nchi yetu. Hivyo basi yatupasa tuipende elimu kwa sababu ni mkombozi wa maisha yetu. Elimu haina mwisho hata kama una umri mkubwa unaweza kujifunza. Daima tukumbuke kuwa elimu huondoa ujinga na ujinga ni mzigo mkubwa sana kwako wewe mwenyewe na pia kwa taifa lako.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection