Jaribu Kutengeneza Utajiri Na Siyo Pesa!

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kuna msemo mwingine ambao unasema “Mwenye Pesa Siyo Mwenzio .”Ukiangalia kwa undani kabisa utashuhudia huo msemo kuwa ni kweli lakini swali la kujiuliza ni muda ambao pesa hizo hudumu. Tumeona kwa macho yetu watu wakifilisika na kubaki kama vile walivyokuwa mwanzo. Haya yote hutokea kwa ile dhana ya kufikiria kuwa pesa ndio kila kitu.

Kutokana na maelezo ya hapo juu tunapata jibu kuwa pesa ni sehemu tu ya utajiri kwa mwanadamu. Ni vyema sana kutengeneza utajiri kuliko pesa. Hii ni kwa sababu utajiri hubeba vitu vingi au rasilimali nyingi, kwa mfano ardhi, majumba, magari, maduka au miradi mbalimbali ambayo inaingiza kipato.

Msingi wa kuandika hayo yote ni kutokana na mtu anapoishiwa hizo pesa au anapofilisika. Inapofikia hatua hiyo ya kufilisika anaweza kuuza chochote alichokuwa nacho na akapata pesa. Hizo pesa zitamwezesha kutatua matatizo yanayomkabili.

Yapo mambo ya kujifunza kutokana na somo hili. Tunajifunza kuwa katika maisha, kuwa na pesa nyingi bila ya kuwa na rasilimali, siyo utajiri. Unatakiwa ukiwa na pesa uzitumie katika masuala ya kuwekeza. Kwa kufanya hivyo, utaweza kuwa tayari kutatua matatizo yanayoweza kukusibu wakati pesa zako zikiyeyuka. Utakuwa na kitu cha kutegemea kutokana na vile ulivyowekeza. Kwa kufanya hivyo, maisha yako yatakuwa yenye raha, amani na utulivu kwa kiwango kilekile ulichokuwa nacho hapo zamani.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Ujinga Mzigo!

Next
Next

Haijawahi Kutokea Mbwa Akaitwa Mbwa Akawa Kichaa.