Haijawahi Kutokea Mbwa Akaitwa Mbwa Akawa Kichaa.

Avelina Hokororo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika maisha unaweza ukaitwa majina mengi tu, mengine ya maudhi, mengine ya kufurahisha, ili mradi tu, utabandikwa majina ya kila aina.!Katika majina hayo, yawezekana mengine yakakuharibia au kukubadilishia tabia yako ambayo tokea mwanzo ilikuwa nzuri.

Kwa mfano unaweza kuitwa mwizi na huku wewe si mwizi kabisa. Cha msingi, hakuna haja ya kukasirika. Kinachotakiwa hapa ni wewe kuendelea na tabia yako ya siku zote, ambayo ni njema. Na hatimaye, wale waliokuita jina hilo la kubandika wataishia kuona aibu na wanaweza wakaacha kukuita hivyo.

Kamwe usibadilishe tabia yako kwa sababu ya kuitwa jina baya la mitaani. Jifunze kupuuzia na kuendelea na tabia yako nzuri. Kwa kufanya hivyo, utawashinda wanadamu wanaopenda kuharibu utu wa wenzao. Hali hii ya kuitwa majina inaweza kusababisha msongo wa mawazo kwa wale ambao wanafanyiwa hivyo.

Mbwa anaweza kuwa na ugonjwa wa kichaa, lakini si kila anayeitwa mbwa anakuwa na kichaa. Inakupasa majina yoyote mabaya utakayoitwa, uachie yapite. Cha msingi, wewe usibadilishe tabia yako iliyo njema. Duniani kuna makero mengi yanayoletwa na wanadamu. Tunatakiwa tuwaelewe binadamu kwani ndivyo walivyo. Hakuna unachoweza kufanya kuzuia hayo, bali ni kuwaeleza hivyo walivyo. Kwa kufanya hivyo, utajiepusha na mengi, ikiwa ni pamoja na matatizo ya afya ya akili

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Jaribu Kutengeneza Utajiri Na Siyo Pesa!

Next
Next

Shinda Tabia Ya Hasira Katika Maisha Yako