Kubali Kupoteza Ili Uende Viwango Vingine

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Katika maisha unaweza kupoteza nafasi, au watu uliowaamini sana. Pengine hata uliweza kufikiri kuwa bila wao maisha au malengo yako hayatafanikiwa.

Sio kila unayempoteza au kila unachopoteza ni hasara kwako. Ni kweli kabisa ukiambiwa neno hili katikati ya maumivu hauwezi kuelewa, ila baada ya muda utagundua lina ukweli ndani yake.

Kuna vitu vingine, lazima upoteze kwanza ili upate vingine. Hali kadhalika, kuna mabadiliko ambayo ni lazima yatokee kwanza ili uwe vile unavyotaka kuwa.

Kuna watu ni lazima waondoke kwenye maisha yako au wawe mbali zaidi ili usogee hatua ya mafanikio.
Usiwang’ang’anie watu ambao unatakiwa kuachana nao. Usilazimishe kuwepo mahali ambapo unatakiwa kuondoka. Usililie vitu ambavyo unatakiwa kuviacha. Kila kitu huja kwa kusudi maalumu, lazima tulijue hilo. Maisha ndivyo yalivyo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Mpe Adui Yako Tabasamu Badala Ya Machozi

Next
Next

Maisha Ni Kutegemeana