Maisha Ni Kutegemeana

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Maisha ya mtu ni fumbo zito. Kila mtu ana umuhimu katika maisha ya mwenzake. Hii ni kwa sababu maisha ni kutegemeana.
Unayemwona hakufai kwa hili leo, anaweza akakufaa kwa lile wakati mwingine. Hata mtu awe maskini kiasi gani, bado anaweza kuwa na umuhimu kwa mtu mwingine, kama siyo kwako. Kuna wakati ambapo anaweza kutoa msaada kwa mwenzake, ukabaki unashangaa.
Pia hata kama wewe ni tajiri wa kujitosheleza usijigambe kamwe kwa kuwaambia watu wewe huhitaji msaada kutoka kwa mtu yeyote. Kwani hiyo siyo kweli kabisa.
Hivyo usimdharau binadamu mwenzio. Kama ni kutoa msaada, wewe toa tu bila masharti, kinyongo au kubagua.
Hata ukiwa na madaraka, kipato kizuri na nafasi ya juu ofisini au mahali popote, hurakiwi kumdharau mtu. Unayemuona hafai leo, kesho unaweza ukamhitaji na anaweza kukusaidia pia. Kwa hiyo, tunapaswa kujenga ushirikiano na wenzetu katika mazingira yoyote yawayo.
Hapa tunapata funzo kuwa, hakuna binadamu aliye kamilika. Hivyo hakuna mtu anayeweza kuishi peke yake. Binadamu sote tunategemeana kwa namna moja ama nyingine. Tumeumbwa ili tusaidiane na hivyo kutegemeana ndio utaratibu wa maisha yetu sisi wanadamu. Hata hivyo isitoshe, safari yetu yetu ni fupi sana. Yatupasa tuutumie muda wetu wa hapa duniani vizuri, kwa kadiri ya uwezo wetu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection