Wakati Mwingine Hawakupendi, Wanakupenda Kwa Kile Ulicho Nacho

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Ni ukweli usiopingika kuwa watu humpenda mtu mwenye nacho. Watu wa aina hii, yaani wale wenye nacho, huwa na marafiki wengi kupita maelezo. Ukweli huu huonekana zaidi kama huyo mtu atakuwa ni mtoaji sana na ambaye anapenda kusaidia watu.
Mara nyingi watu hupenda kuwafuatilia watu wenye hali hiyo, yaani wale wenye nacho. Watu hawa hujitahidi kuonyesha upendo wa ajabu na pia huwamwagia sifa nyingi watu ambao wanacho.
Maisha ya mwanadamu ni yale ya kupanda na kushuka, hilo halikwepeki. Pale ikitokea kuwa mambo yameenda vibaya, basi wale watu wote waliokuwa wakimfuatilia kwa mbwebwe na vifijo,
hutokomea kabisa. Kuanzia hapo, hakuna mtu atakayemsogelea tena. Sababu kubwa ya kukimbiwa ni kutokana na ukweli kwamba hana kitu tena na hana msaada kwao tena. Watu hao watatokomea mmoja baada ya mwingine. na watakuwa hawana mpango na wewe tena.
Endapo hapo nyuma ulikuwa umeomba msaada kutoka kwao, sasa itabaki kuwa ni kejeli tu na masimango. Huu ndio ulimwengu ulivyo, ulimwengu tunamoishi sisi wanadamu.
Kwa kawaida, sisi binadamu hatuna shukurani hata kidogo. Ukitenda wema usitegemee kurudishiwa fadhila. Pamoja na yote, wewe tenda mema tu huku ukijua kuwa shukurani hazitakuwepo. Hali kadhalika, tuwe na kiasi katika kusaidia watu maana
binadamu ni wa ajabu, wana matatizo na shida nyingi. Siyo rahisi kuwajua, kwani hubadilika kila uchao.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection