Mpe Adui Yako Tabasamu Badala Ya Machozi

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Unaporuhusu uchungu na maumivu ndani yako ni rahisi sana kuchoka na kukataa tamaa. Usibebe kila kitu, na wala usichukulie kila kitu kwa uzito, utaelemewa. 

Kuna mambo unahitaji kuyapuuzia. Usitake kujua kila unachofanyiwa na adui zako na watesi wako. Mengine acha yapite kama vile hujayasikia na kama vile, hayakuhusu.

Unapomuonesha adui yako machozi yako na uchungu, unasababisha adui ajisifie, ajione yeye ni bora na kwamba ‘amekuweza’.

Lakini unapompuuza adui yako, unamfanya akose nguvu na hatimaye atachoka kukufuatilia. Kwa hiyo usiubebeshe moyo wako na nafsi yako mizigo isiyo ya lazima. Kwa kubeba kila ambacho adui yako anakufanyia, utajichosha.

Jipe utaratibu wa kupuuzia baadhi ya mambo ili moyo na nafsi yako viwe huru. Binadamu ni kiumbe wa ajabu, usimuendekeze, utajiumiza bure.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Anayekukosoa, Anakujenga!

Next
Next

Kubali Kupoteza Ili Uende Viwango Vingine