Anayekukosoa, Anakujenga!

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Ni kawaida ya watu wengi kupenda kuonekana kuwa wako mbele sana katika kila jambo wanalolifanya. Hakuna mtu anayetaka kuonekana kuwa hawezi.

Ni ubinadamu kabisa kwa mwanadamu kupenda kusifiwa kuliko kurekebishwa. Inawezekana kabisa kuwa mtu anafanya mambo ambayo hayawapendezi watu, lakini anakuwa hayuko tayari kurekebishwa. Endapo atatokea mtu wa kumkosoa, basi ataanza visa kuhusu huyo mtu na hata anaweza kuanza kumsema vibaya. Mara nyingi, hapo ndipo chuki huanzia. 

Katika maisha yetu, inatupasa kukubali na kuwa tayari kukosolewa. Kukosolewa kunamtengeneza mtu.  Unapokubali kukosolewa unakuwa na uhakika wa maisha ya baadae. Tukumbuke kuwa maisha ni kama ngazi kubwa, usipopanda vizuri, utateleza na kuanguka. Na ukianguka utabaki kujilaumu, oh fulani aliniambia, nk. Mwisho inabaki ni majuto tu.

Kubali kuonywa. Usimkasirikie anayekuonya maana anakuelekeza namna ya kuenenda na mwisho utafanikiwa katika hilo jambo. Hakuna aliyefanikiwa bila ya kupitia misukosuko. 

Tupende kuelekezwa, tusichukie tunapoonywa maana hata maandiko matakatifu yanatusihi kusikiliza maonyo na kuyatendea kazi kwani ndipo ushindi wetu ulipo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Usitegemee Uzuri Wako Maana Kuna Siku Utazeeka

Next
Next

Mpe Adui Yako Tabasamu Badala Ya Machozi