Usitegemee Uzuri Wako Maana Kuna Siku Utazeeka

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Wako mabinti zetu wengi ambao wanajiona ni wazuri kwa umbo na sura. Watu hao mara nyingi hujiona kuwa ni bora zaidi kuliko wengine. Na huwa wanapenda hata kuchagua ni nani watakuwa wenzi wao.
Wengi hupenda kutafuta watu wenye uwezo na ambao wamefanikiwa katika maisha. Lakini huwa hawajali au hawapendi kujua kuwa hao wanaowapapatikia wamefikaje pale walipo. Tamaa hiyo inawafanya kuwa na wapenzi wengi. Hapo kunakuwa na mashindano, kila mtu anavutia kwake ili aonekane mzuri zaidi ya mwingine.
Tabia hii ya kuruka ruka huwafanya mabinti wengi wasahau kuwa kuna kuzeeka. Kadri wanavyozidi kujichelewesha na umri nao unazidi kuyoyoma.
Kikubwa kinachotakiwa ni kujiheshmu na kuwa na tabia nzuri. Kwa kufanya hivyo ndipo unaweza kuimarika. Hali kadhalika, Muumba wako naye hatimaye, atakupatia yule aliyekuandalia kuwa mwenza wako, yule ambaye atakuwa wako milele.
Kuna mifano hai mingi ya mabinti kujidanganya. Tunaona kwenye mtandao kinachoendelea kuhusu kijana aliyejirusha kutoka ghorofani. Eti kuna mabinti zaidi ya wawili, kila mmoja anajiona kuwa ana haki zaidi ya kutambuliwa kuwa ndiye aliyekuwa mwenza wa huyo kijana. Lakini kwa bahati mbaya, katika hao mabinti wawili, hakuna ambaye alijaliwa kuzaa na yule kaka. Inasemekana mmoja kati yao ameishi na huyo kijana kwa miaka minne, na mwingine miaka mitatu. Kuna mwingine aliishialipiwa hata mahari, lakini hakuna aliyezaa nae. Hali hii imeleta vurugu tosha.
Haieleweki kwa nini yule kaka aliamua kuishi maisha ya namna hiyo. Kila binti aliyehojiwa anaongea lake, anavutia upande wake. Yaonekana kijana huyu alikuwa ni kama tegemeo la kila mmoja wao. Kifo chake kimekuwa ni pigo kubwa kwao. Nguzo imeanguka kwa wote.
Kila mmoja amebaki kujilaumu na kujiuliza, “kwa nini alijichelewesha kusonga mbele?”Kijana alikuwa mtanashati, mtoaji, lakini siyo muoaji. Mabinti waliponzeka na utanashati wake, waliehuka na utoaji wake. Leo wanalia, wamebaki na majuto.
Tunakumbushwa kuwa tusipende vya kuvikuta, bali ni vema ukaanza naye toka kwenye sifuri, mkajenga pamoja taratibu, lakini mwisho wa siku mtakavyochuma vitakuwa vyetu nyote wawili. Mabinti wanaaswa kuondoa kiburi cha uzuri. Tabia nzuri ndio iwe ngao ya maisha ya mtu yeyote.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection