Furaha Ni Kama Marashi Kwani Huongeza Maisha

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Wahenga wa kale walisema, "Kitu furaha ni sawasawa na marashi”, kwani huwezi kujipulizia wengine wasisikie harufu yake. Hii inajidhihirisha wazi kwamba ukiwa na furaha huwezi kuificha kwani mtu yeyote atakayekuona atatambua kuwa umefurahi au una furaha. Basi, endapo wewe umefurahi, jitahidi na watu wengine nao wafurahi kutokana na furaha yako.

Hata siku moja usikubali kufurahi au kuruhusu kupata raha baada ya kuona shida, maumivu, machungu au maanguko ya mtu mwingine. Yaani usifurahie kuteseka kwa mwenzio, kwa mfano, kufiwa, kupata ajali, kuuguliwa, kupata mikosi, uchumi kuporomoka, kuibiwa au kufeli shule.

Hapa tunapata funzo kuwa, ukiwa na furaha siku zote mshirikishe au mwambukize mwenzio, ndugu yako, rafiki au jirani kwani furaha huongeza au hurefusha maisha ya binadamu, kinyume chake ni makasiriko au hasira ambazo husababisha msongo wa mawazo, na kusononeka ambapo hatima yake ni maamuzi hasi kama vile, kujinyonga, kujirusha dirishani au kujidhuru kwa njia moja au nyingine. 

Hivyo, sisi kama binadamu, furaha ni kitu muhimu sana inatakiwa iwe sehemu ya maisha yetu ya kila siku kwa ajili ya kutuongezea siku zetu za kuishi hapa duniani.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Nyani Akiumwa Ukimpa Dawa Akipona, Jiandae Mahindi Yako Kuliwa

Next
Next

Usitegemee Uzuri Wako Maana Kuna Siku Utazeeka