Nyani Akiumwa Ukimpa Dawa Akipona, Jiandae Mahindi Yako Kuliwa

Avelina Hokororo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Nyani ni mnyama anayekaa porini. Anafanana na ngedere au kima. Anakula sana mahindi yakiwa shambani. 

Kuna ndugu anaweza kuja kwako akiwa hoi kimaisha, hata hela ya kula hana. Safari yake ni kuja kuomba msaada. Unampokea na kukaa naye nyumbani kwako. Anakula kile ambacho Mungu amekujalia hapo nyumbani pako. 

Baada ya siku kadhaa unampa mtaji wa pesa. Anaanzisha biashara yake ukiwa naye hapo nyumbani pako. Hatimaye anafanikiwa. Anahama pale nyumbani pako na kwenda kujitegemea sehemu nyingine. 

Kutokana biashara ile uliyomuanzishia, maisha yake yanakuwa ya juu kuliko hata ya kwako. Sasa badala ya kukushukuru, anaanza kukudharau na kukutangazia ubaya kwa watu kuwa ulikuwa unamnyanyasa sana. Anakuona kuwa hufai kwa lolote, na kwamba wewe si chochote mbele yake.

Simulizi hii inafundisha kuwa siyo wote utakaowasaidia watakuja kukumbuka kwa mema yako. Mfano wa nyani mgonjwa kwenye simulizi hii, ni yule mtu aliyekuja kuomba msaada kwako. Kwa huruma unampa dawa (pesa) akapona. Sasa baadaye anakuja kukushambulia kwa dharau za kupitiliza. 

Hii ni sawa na usemi usemao: “Tenda wema uende zako,  usingoje shukurani”. Kuna binadamu wengi ambao wana tabia kama hii ya utovu wa shukurani. Yatupasa tuwavumilie tu na kutowajali kwani wako wengi hao. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Utaula Wa Chuya Kwa Uvivu Wa Kuchagua

Next
Next

Furaha Ni Kama Marashi Kwani Huongeza Maisha