Achana na Neno Haiwezekani Upate Mafanikio

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Ukitaka kupata mafanikio maishani mwako usiwe na mazoea ya kutumia neno ‘haiwezekani’. Mojawapo ya udhaifu mkubwa wa binadamu ni kuzoea kutamka neno hili la haiwezekani. Mara nyingi watu wenye neno haiwezekani midomomi mwao ndio ambao huwa hawafanikiwi katika maisha.

Ukweli ni kwamba, siyo kuwa mambo hayawezekani bali ni wewe usiyejaribu, usiyethubutu, usiyejiongeza na usiyechapa kazi. Usipofanya hayo, mafanikio hutayaona, yatakuwa hayana mlango wa kupita.

Tatizo la binadamu tulio wengi ni kukata tamaa. Tunashauriwa kuwa, kamwe hatutakiwi kukata tamaa. Daima tukumbuke kuwa mabaya yamejipanga foleni, yako mbele yetu yakitusubiri maishani mwetu. Tusipokuwa waangalifu na matumizi yetu ya maneno, ama tunapokata tamaa, tutajikuta tunakaribisha mabaya mengi yatutokee.

Watu wanaofanya vitu vikubwa ni wale waliojaribu yale ambao wengine walisema hayawezekani. Wao waliondoa hofu na wakafanikiwa. Yatupasa tuachane na maneno yatakayotufanya tusisonge mbele. 

Kupata na kukosa ni mambo ya kawaida. Hakuna lisilowezekana duniani. Kila kitu ni kujaribu na kuweka bidii, utafanikiwa. Kumbuka, kinywa kinaumba, ukisema haiwezekani, inaweza isiwezekane kweli kwa  sababu ulijitamkia mwenyewe.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Kuvunjika kwa Koleo, Sio Mwisho wa Uhunzi

Next
Next

Jifunze Kutotangaza Shida Zako